Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba akiongea na Mkurugenzi mkuu wa Kiwanda cha kusindika Mafuta ya Alizeti Khalidi Ally (kulia )
Mkuu wa Mkoa akipata maelezo katika ghala la Mshudu.
Khalid Ally akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa baada ya kumaliza ziara yake fupi huku akiipongeza Serikali kwa kuwajali wanachi wake hasa wakulima.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter
Serukamba amesema kuwa serikali mkoani humo imejipanga kuhakikisha unaunga mkono wawekezaji wa ndani ya mkoa huo kwa lengo la
kutengeneza ajira na fursa kwa wazawa na maendeleo ya Mkoa huo.
Serukamba alitoa kauli hiyo katika
ziara yake alipotembelea Ujenzi wa kiwanda cha usindikaji Alizeti cha Wild FLOWER
Grant & Oil Mills Company Limited
kilichopo Manispaa ya Singida.
Alisema kuwa serikali ya Mkoa inaunga mkono uwekezaji huo kutokana na
Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea
kuleta Mbolea ya Ruzuku ili zao hilo
liweze kuzalishwa zaidi Mkoani hapa kutoka na zao hilo kuwa ndiyo zao kuu la
Biashara.
SERUKAMBA alisema kuwa tunataka kuona mkoa wa Singida unaingia kwenye
Ramani ya taiafa katika uzalishaji wa Mfuta ya Alizeti na Mashudu ili kuongeza
kipato cha Mkoa na Serikali kupunguza uagizaji wa Mafuta ya kupikia kutoka nje.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wild Flower Grant & Oil Mill Company
Limited Khalid Ommary Ally akiongea na Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kiwanda hicho kitaghalimu zaidi ya Dola Mil 24 sawa na zaidi ya Bil 60 za kitanzania
hadi kukamilika kwake.
Khalid alisema kuwa Ujenzi wa Mradi huo unatarajia kukamilika mwezi
Desemba Mwaka huu na kuzalisha zaidi ya
Lita 75,000 za Mafuta ya Alizeti kwa Siku, pamoja na kuajiri zaidi ya
wafanyakazi 400,hadi 500 na kipaumbele kikiwa ni wakazi wa Singida.
0 Comments