Jengo la Utawala la Ofisi ya Manispaa ya Singida linalo jengwa Mwenge mjini Singida.
Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba(katikati)akikagua eneo la mradi katika Hospitali ya Manispaa baada ya kupata maelezo.
Zaidi ya shilini bil 3 zitatumika katika ujenzi wa jengo la Utawala la Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiwa ni fedha zilizotolewa na serikali.
Akisoma taarifa ya Mradi huo mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Singida alipotembelea Miradi ya Maendeleo ya Manispaa ya
Singida kaimu Mhandisi kutoka Ofisi ya Manisapaa Karisto Mligo amesema kuwa ujenzi wa Mradi huo
mpaka sasa umeshatumia zaidi ya Mil 878
likiwa katika hatua ya ghorofa ya pili.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri
ya Manispaa Singida Jeshi Lupembe alisema kuwa kwa sasa vifaa vya kukamilisha
ujenzi huo vimesha nunuliwa mpaka sasa tunasubiri ni mfumo wa malipo ya fedha ili tuweze kuendelea na ujenzi na kulipa fedha
za mkandarasi zaidi ya sh Mil 51.l
Aidha Mkuu wa mkoa wa Singida Petert
Serukamba akiongea baada ya kukagua jengo hilo ameutaka uongozi wa Manispaa kuhakikisha
wanakamilisha jengo hilo kwa wakati, huku akiagiza halmashari zote Mkoani Singida kutumia wakandarasi wenye
uwezo ili kukamisha miradi kwa wakati .
Mkuu wa Mkoa Peter serukamba kabla ya
kutembelea jengi hilo la utawala Manispaa ya Singida pia ametembelea Hospitali
ya Manispaa ya Singida na kupata taarifa ya mwenendo wa Ujenzi na Ukarabati
baada ya kupata fedha Tzs Mil 500 kutoka serikalini.
Akiowa katika Hospitali hiyo mkuu wa
mkoa ameuwagiza uongozi wa Manispaa kuhakikisha vibali vya ujenzi wa
miundombinu mbalimbali ya Hospitali hiyo unaanza mara moja.
0 Comments