Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamba akiongea na wakuu wa idara mbalimbali wa halmashauri ya Itigi Wilayani Manyoni.
Watumishi wa Halmashauri.
Maofisa
kilimo Mkoani Singida wameagizwa kupima afya ya ugongo kwenye mashamba ya
wananchi na kuwashauri wakulima juu ya mazao yanayofaa kulimwa kulingana na
afya ya shamba husika ili kulima kilimo chenye tija.
Akizungumza
na viongozi wa halmashauri za Wilaya ya Manyoni na Itigi mkuu wa mkoa wa
Singida Peter Serukamba amesema imefika wakati wa kuwapima viongozi kwa
kutekeleza maagizo anayoyaagiza ili kuwanufaisha wakulima
Serukamba amesema hakuna namna nyingine ya kuongeza uzalishaji katika kilimo
bila kutumia mbegu bora na matumizi sahihi ya mbolea za ruzuku zinazotolewa na
serikali kwa lengo la kuwainua wakulima
Katika hatua nyingine Serukamba amesema viongozi wote wafanye kazi katika idara
zao kwa weledi na kuacha tabia ya kuwabebesha wengine mzigo wa majukumu yote
huku wengine wakikwepa wajibu wao.
Nao
wataalamu wa kilimo wamesema elimu ya matumizi bora ya mbolea inaendelea
kutokewa kwa wakulima ambapo idadi ya wakulima imeongezeka kwa msimu huu wa
kilimo ikilinganishwa na msimu uliopita.
0 Comments