Mkuu wa mkoa wa Singida akiongea na viongozi kutoka wilayani.
Meya wa Manispaa ya Singida Yagi kiaratu akichangua juu ya usambazaji wa Mbegu unayoendelea katika eneo lake hasa pembezoni mwa mji wa Singida.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni Hussein Simba naye akitoa maoni yake sambamba na Ushauri kwa Serikali.
Wakirugenzi wa halmashauri ya Iramba na Manispaa ya Singida wakifuatilia hotuba.
Afisa Utumishi kutoka wilaya ya Singida Dc akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi.Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA amewataka Viongozi wa
Halmashauri zote za Mkoa huo, kuhakikisha Mbegu za Alizeti zenye Ruzuku,
zinasambazwa kwa wakulima.
Akiongea katika Kikao kazi cha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote Mkoa huu, kikao ambacho kilijadili Agenda mbalimbali za maendeleo ya Mkoa huo.
SERUKAMA aliwataka Viongozi wa Halmashauri zote na Maafisa Ugani kutumia siku Sita (6) kuhakikisha Mbegu hizo sinasambazwa na kuwafikia wakulima katika Msimu huu wa Kilimo.
Nao wajumbe wa Kikao Kazi hicho walisema ni vyema kuutumia
Msimu huu wa Kilimo kubaini changamoto zilizojitokeza katika Misimu iliyopita
ili kuzitatua kwa ajili ya misimu ijayo ya kilimo.
0 Comments