Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamba akisisiza jambo katika kikao kazi.
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Fatum Mganga akitoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi.
Wakuu wa Wilaya wa Manyoni Kimilembe Lwota (kulia)na Thomas Apson wa Ikungi katika kikao hicho.
Wkuu wa Idara kutoka wilaya za mkoa wa Singida wakifuatilia na kupata maelekezo juu ya Miradi hiyo.
Zaidi ya Bil 5 zimepokelewa kutok
Serikali kuu, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Miradi ya Maendeleo
Mkoani Singida ikiwemo Madarasa na Umaliziaji wa Miradi ya Afya huku Miradi
hiyo ikitakiwa kukamilika ndani ya Siku 90.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Peter
Joseph Serukamba, amewaagiza wakuu
wa wilaya na wakurungenzi wote Wa halmashauri za Mkoa wa singida, kuhakikisha
fedha zote za Miradi zinapelekwa mapema
kwenye maeneo ya Miradi.
Serukamba ametoa agizo hilo katika
Kikao kazi Cha kupokea taarifa mbalimbali ikiwemo uandikishwaji wa wanafunzi
shuleni, utekelezwaji wa Miradi ya maendeleo, usambazwaji wa mbegu na mbolea, na
alitumia fursa hiyo kuwaagiza wakuu wa wilaya na wakurungenzi kuhakikisha fedha
zote zilizotolewa na serikali Kuu zinafika mapema katika maeneo ya Miradi na
ujenzi ufanyike kwa wakati.
Kwa upande wao wakuu wa wilaya za
Ikungi na Manyoni, walisema wameyapokea maelekezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa ,
na kukiri kuwa kitendo Cha fedha
hizo kupelekwa katika maeneo ya Miradi
itarahisisha kununuliwa mapema kwa vifaa vya ujenzi.
0 Comments