DC APSON APELEKA MATURUBAI 22 KIJIJI CHA MWAKALANJA (W) IKUNGI.

 

                                                        Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson.

KUTOKANA  na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi mwaka huu 2024 Mkoa wa Singida umekuwa na mvua kubwa kuliko mwaka uliyopita 2023 kutoka mm80 hadi 120mm kwa sasa na kufikia mm180 hadi Aprili 2024 hivyo maeneo mengi yamezingira na maji na kusababisha baadhi ya nyumba zimeanza kuporomoka kabisa na zingine kuwa na nyufa.

Kutokana na hali hiyo mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sasa mkoani Singida Kijiji cha Mwakalanja kata ya Mgungira wilayani Ikungi kimezingirwa na maji nyumba 22 zimebomoka kabisa na zingine 33 zimekuwa na nyufa na mpasuko hivyo wakazi 22 wa nyumba hizo hawana makazi.

“Nyumba nyingi zimetoka na maji, mabwawa yamejaa na mito yote imejaa maji nab ado mapema sana haijulikani hali ya Aprili hali itakuwaje”

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani tayari imeanza kupeleka misaada kwa familia zilizokubwa na mafuriko katika eneo hilo kukabiliana na majanga yake maturubai 22 yameshapelekwa nab ado taratibu zingine zinaendelea inasemekana mawasiliano yameanza kuwa magumu na matatizo ya kiafya yanaweza yakaanza kujitokeza.

Akitoa taarifa hizo juzi juu ya hali ilivyoasjitokeza wiki iliyopita kwa gazeti hili Afisa Mtendaji wa kata ya Mgungira Abdallah Simion amesema Kijiji chote cha Mwakalanja na vile vya majirani vimezingirwa na maji ya bonde kuu la Wembere kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kila siku.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mgungira kata ya Mgungira Hussein Ng’oni amesema ekari Zaidi 3,000 za mazao ya chakula ya msimu huu wa kilimo zimekumbwa na maji na nyumba nyingi zimezingirwa na maji.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson baada ya kupata taarifa za mafuriko Kijiji cha Mwakalanja amepeleka maturubai 22 na baadae atawapelekea wananchi wa Kijiji hicho mahema kwa sababu hali iliyopo sasa siyo nzuri kiafya na chakula nab ado mvua kubwa zinaendelea kunyesha.

Uchaguzi wa gazeti hili umebaini vijiji vingi vya maeneo  hayo ya mbugani vitakubwa na mafuriko hasa mgungira, iyumbu, Magungumuka, Kaugeri, Mwasusu na Mduguyu, hata hivyo Ufana haitaachwa na mafuriko hivyo nyumba nyingi zilizojengwa kwa kiwango cha chini zitabomoka.

Hata hivyo wakazi wa kata za Igombwe, Mgungira, Iyumbu  na Mwaru wamesema japokuwa mvua za mwaka huu ni kubwa katika maeneo hayo yenye misitu ya asili hali ya mazao ya chakula itakuwa nzuri sana na kutakuwepo na samaki wengio mwaka huu kwenye bonde kuu la  Wembere linaloanza Iyumbu, Mgungira, hadi Kaugeri.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments