MWILI WA CLEMENT MTENGA WATUA NCHINI.

 Mwili wa marehemu Clemence Mtenga, Mtanzania aliyekuwa akiishi nchini Israel, unatarajiwa kuwasili Tanzania kesho Ijumaa usiku.

Ijumaa iliyopita, Serikali ya Tanzania ilidhibitisha kifo cha kijana huyo na kueleza kuwa kilitokana na shambulizi lililofanywana Oktoba 07 nakundi la Kipalestina la Hamas.

Ubalozi wa Tanzania mjini Tel Aviv umeidhibitishia BBC kwamba mwili wa marehemu utawasili siku ya Ijumaa katika jiji la kibiashara la Dar es salam ndugu na jamaa wa marehemu Clemence Mtenga, Mtanzania aliyekuwa akiishi nchini Israel, unatarajiwa kuwasili Salaam ikiwa ni siku moja baadaya jamaa na marafiki mbalimbali kuaga mwili huo katika balozi ya Tanzania.

Alex Kalua, Balozi wa Tanzania nchini Israel, anasema marafiki na jamaa wa Clemence walikusanyika jana na kumuaga marehemu Mtenga.

Anasema, "Marafiki wa Kitanzania walimuaga marehemu Mtenga, na hivyo tunatarajia mwili wake utafika Tanzania Ijumaa usiku kisha taratibu zingine zitaendelea kutoka hapo."

Mpaka sasa familia ya marehemu Mtenga bado haijathibitisha juu ya mipango ya mazishi.

Kwa Mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya Idara ya mambo ya nje ya Tanzania,Mtenga alikuwa nchini Israel kwa ajili ya programu ya mafunzo ya ndani, na alifariki Oktoba 7.

Hata hivyomamlaka ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu Mtanzania Joshua Mollel ambaye anadaiwa kushikiliwa mateka. Mamlaka ya Israel awali ilithibitisha kuwa Mollel alikuwa miongoni mwa watu zaidi ya 200 wanaoshikiliwa mateka huko Gaza.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments