SINGIDA
Mratibu wa Elimu kwa njia ya masafa Fortunata Tarimo kutoka shirika lisilo la kiserikali la INADES FORMATINO TANZANIA kutoka Dodoma akitoa Elimu kwa wanavikundi vya Mkombozi na Huruma kotoka kijiji cha Kinyamwenda.
wanakikundi cha Huruma wakiangalia vitabu hivyo baada ya kupatiwa ufafanuzi.
wanavikundi wakiendelea na usomaji wa vitabu hivyo.
Fortunata Limo akifafanua jambo kwa wanavikundi baada ya kuwapatia vitabu mbalimbali wanavikundi hao.
Katika kuahakikisha mwananchi, wakulima na wajasiliamali wanapata elimu na ujuzi mbalimbali katika kukuza uchumi shirika lisilo la serikali la maendeleo ya kiuchumi na kijamii la INADES FORMATION TANZANIA limeanzisha mpango wa kutoa elimu kwa njia ya masafa.
Akiongea na
standard radio Bi Fortunata Tarimo mratibu wa mafunzo kwa njia ya masafa
amesema mafunzo hayo yamegawanyika
katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo pamoja na uongozi na maendeleo
Bi,Fortunata ametaja baadhi ya vijitabu ambavyo wanavyo na vinatumika ilikutoa elimu kwa jamii.
Aidha Bi Fotunata amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi kwa jamii au vikundi mbalimbali nchini ili kuimarisha shughuli zake za kila siku na kuharakisha katika kuleta maendeleo.
Akizungumzia
juu ya changamoto wanayokutana nayo katika utoaji elimu kwa njia ya masafa Bi
Fortunata ameongeza kuwa ni namna bora ya usafirishaji kwa njia ya posta pamoja
na baadhi ya maeneo mengine kutokuwepo na huduma ya posta na kuwafanya wadau
kusafiri kutoka vijijini kuja mjini kufuata huduma hiyo ya posta wakati
mwingine kusababisha upotevu wa vitabu nivyo.
0 Comments