Andres Iniesta amekamilisha huduma
yake ya kuichezea Barcelona katika mechi ambayo Barcelona imewaadhibu Real
Sociedad wakati wa mechi za mwisho za La Liga.
Iniesta ameagwa kishujaa kwani mashabiki waliunda maandishi ya
kumuaga, uwanja ukawashwa taa maalumu kwa ajili yake na akajitokeza machozi
yakimtoka akasema, nilifika hapa nikiwa mtoto sasa ninaondoka nikiwa mwanaume,
nitawaweka katika moyo wangu milele.
Sherehe za kumuaga zimefana na kuwaacha hata wachezaji wenzake
akiwemo Messi wakibubujikwa na machozi huku mashabiki wakiwasha taa za Simu zao
na vifaa vingine katika Giza la Uwanja ili kuonesha heshima kwa mchezaji huyo.
Wachezaji wote walivalia Jezi namba nane yenye jina la Iniesta.
Mashabiki
walijiunga pamoja kuunda neno Infinit Iniesta
yaani Iniesta
Milele, naye alipopewa kipaza sauti
amesema,
"asante kwa wachezaji wenzangu, kila mmoja.
Nitawakumbuka
kila mmoja wenu.
Na asante sana mashabiki, kwa mapenzi yenu,
kila kitu
mlichonifanyia
tangu nilipofika hapa nikiwa mvulana
mdogo.
Ninaondoka
nikiwa mwanaume. Nitawaweka moyoni
mwangu
milele"
Iniesta mwenye miaka 34 amekaa Barcelona kwa miaka 22 na kutwaa
mataji makubwa 22 katika miaka 16 aliyochezea Timu ya wakubwa kwani alianzia
katika timu ya watoto klabuni hapo.
0 Comments