Godwin Gondwen akitoa taarifa ya mbio za mwenge katika wilaya yake ya Singida Dc
Mkuu wa Mkoa wa Singida akiongea katika mapokezi ya Mwenge katika kijiji cha Itaja
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Queen Sendiga akiongea wakati wa makabidhiano ya Mwenge.
Wakuu wa Wilaya ya Singida wakiwa katika mapokezi ya Mwenge.
Singida
Mwenge wa
Uhuru umeanza rasmi mbio zake katika mkoa wa Singida, baada ya kumaliza ziara
ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Manyara.
Akizungumza
mara baada ya kupokea Mwenge huo katika viwanja vya Kijiji cha Sagara, Kata ya
Itaja, Wilaya ya Singida, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mheshimiwa Godwin Gondwe,
alisema kuwa mkoa huo umejiandaa kikamilifu kuhakikisha Mwenge wa Uhuru
unatembelea miradi ya maendeleo kwa mafanikio.
"Singida
tumejipanga kuhakikisha Mwenge wa Uhuru unakimbizwa kwa usalama, huku ukikagua
miradi ambayo ina tija kwa wananchi wetu."
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, akitoa taarifa ya
Mwenge wa Uhuru katika mkoa wake, alisema kuwa Mwenge huo umetembelea miradi 51
yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 71.3.
"Tumefanikisha
ukaguzi wa miradi 51, na tunaamini utekelezaji wake utaendelea kuleta maendeleo
endelevu kwa wananchi wa Manyara."
Naye,
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi, amepongeza uongozi wa
mkoa wa Manyara kwa usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo, akiutaja kuwa
ni mfano wa kuigwa.
"Hongereni
Manyara kwa kazi nzuri. Miradi yenu inaonyesha matumizi mazuri ya rasilimali na
dhamira ya kweli ya maendeleo."
Mwenge wa
Uhuru unatarajiwa kutembelea miradi 52 katika mkoa wa Singida yenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 62, ukiwa na ujumbe wa kuhamasisha maendeleo,
mapambano dhidi ya rushwa, magonjwa, na kushiriki uchaguzi kwa amani na
utulivu.
0 Comments