 |
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka akifafanua jambo wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Yurason wilayani Mkalama wakati wa upandaji miti, ni katika zoezi la upandaji miti linaloratibiwa na Standard Fm 90.1 ya Singida huku zoezi hilo awali lilizinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi na kuanzia wilaya ya Ikungi,Iramba na sasa ilimemalizika Mkalama kabla ya kwenda wilaya ya Singida., |
 |
wananchi wakipata maelekezo kabla ya kuanza upandaji wa miti hiyo. |
 |
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka akipanda mti. |
 |
Mwakirishi wa mkurugenzi wa Standard Fm Ally Juma akipanda mti. |
 |
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga akipanda mti. |
 |
Mshauri wa Jeshi la Mgambo wilya ya Mkalama akipanda mche wa mti. |
 |
Waandishi wa habari wa Teddy Mande na Revocatus Phinia wakijadili jambo wakati zoezi hilo la upandaji miti likiendelea. |
 |
Kaimu OCD wa wilaya ya Mkalama akionyesha namna ya kupanda mti. |
 |
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Standard Fm Teddy Mande akishiriki kikamilifu katika upandaji miti. |
 |
Festo Sanga mwandishi wa habari wa Standard FM akipanda mche wa mti. |
Mkuu wa
wilaya ya mkalama mkoan Singida mhandis Jackson Masaka ameipongeza standard
redio kwa kuanzisha kampen ya kuufanya mkoa wa singida kuwa wa kijani kwa
kupanda miti.
Mhadis
Masaka amesema hayo akiwa ofisini kwake wakati akitoa taarifa fupi juu ya
upandaji miti katika wilaya yake kabla ya kuanza rasmi zoezi la kupanda miti
katika kijiji cha Yulanson.
Masaka
amesema kampeni hiyo ya upandaji miti itasaidia sana kuufanya mkoa wa Singida
kuwamfano wa kuigwa katika maeneo mbalimbali.
Amesema
jitihada mbalimbali za wadau zinahitajika iliuweza kupanda miti ya kutosha
kwalengo la kuondoa hali ya ujangwa.
Ameiomba standard redio kuendeleza kampeni hii kwani inaendana
na kampeni ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia
Suluhu Hassan ya kuifanya Dodoma ya kijani.
Tuandikie Maoni Yako Hapa
0 Comments