HECTA 6000 ZATENGWA KUJENGA VIWANDA SINGIDA

Katibu tawala mkoa wa Singida Dr Angelina Lutambi

Jumla ya  Hecta  6000 zimetenga katika mkoa wa Singida  kwa lengo la kujenga  viwanda  mbalimbali  ili kufikia dhima ya  serikali ya viwanda


 Akitoa  taarifa  kwa kamati  ya  bunge  biashara viwanda na mazingira  katibu tawala  mkoa wa Singida Dr Angelina Lutambi  amesema lengo la kutenga hekta hizo  ni kuunga mkono jitihada  za serikali kuelekea  uchumi wa kati

Amesema tayari  halmashauri zote za mkoa wa Singida zimetenga maeneo ni rafiki  kwa uwekezaji huo

Aidha akisoma  taarifa ya  utekelezaji wa kazi  zao  meneja wa SIDO  mkoa wa Singida Bi Shoma Kibende  amesema wao  wameendelea kuhamasisha  wananchi juu  ya ujenzi  wa viwanda. 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments