| Mh Suleimani Sadiq Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Viwanda ,Biashara na Mazingira akifafanua jambo. |
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesusia
kupokea taarifa ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), huku ikitoa onyo
kwa wateule wa Rais John Magufuli kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwa kasi
inayohitajika.
Agizo hilo limetolewa leo Machi 15, 2018 mkoani Singida ambapo
kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Sadiq walipofika kutembelea
viwanda kadhaa mkoani humo na mwenyeji wao alitakiwa kuwa ni Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Akizungumzia leo, Sadiq amesema kamati ya Bunge inapotembelea
anapaswa kuwapo waziri, naibu waziri au katibu mkuu, lakini “tumemkuta naibu
katibu mkuu na maofisa wengine wa wizara na wale wa Sido, ambao hawakuwa
wamejindaa na tumeikataa taarifa yao.”


0 Comments