Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt Elipidius Baganda akifungua kikao kazi hicho.
SINGIDA:
Kikao kazi
cha mrejesho wa Mradi wa Shule Bora kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Singida, kikilenga kujadili utekelezaji wa mradi huo, pamoja na
kuangalia mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt. Elipidius Baganda, amesema kuwa mradi huo umeleta matokeo chanya kwa sekta ya elimu mkoani humo, ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa majengo, ujenzi wa shule mpya, na kuboresha miundombinu ya elimu.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Anna Tutuba,
pamoja na Afisa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari wa wilaya hiyo Zipporah
Simwanza, wamesisitiza kuwa programu ya Shule Bora imejipambanua kuhakikisha
inaleta mabadiliko ya kweli. Wamewataka wakurugenzi wote wa halmashauri mkoani
Singida kusimamia kwa makini fedha zinazotolewa ili kuhakikisha zinatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mratibu
wa Shule Bora Mkoa wa Singida Fredrik Ndahani, amesema kikao hicho kimekuwa
jukwaa muhimu la kutathmini utekelezaji wa mradi huo, kujadili mafanikio
yaliyopatikana, pamoja na kutafuta suluhu za changamoto zilizojitokeza, hususan
katika usimamizi wa fedha.








0 Comments