1. Bw. ALLY SALUM HAPI (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya AMINA
MASENZA ambaye amestaafu.
2. Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameteuliwa
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu SALUM
KIJUU ambaye amestaafu.
3. Bw. ALBERT CHALAMILA ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Bw. AMOS GABRIEL MAKALA ambaye amehamishwa
na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL
MUHUGA amestaafu.
4. Brigedia Jenerali NICODEMAS ELIAS MWANGELA
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi ya Luteni Mstaafu
CHIKU GALLAWA ambaye amestaafu.
Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya
wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa
kama ifuatavyo:
1. Bw. KESSY MADUKA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MADENGE
2. Bw. ABOUBAKAR MUSSA KUNENGE ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Bibi THERESIA MMBANDO.
3. Bw. DAVID KAFULILA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Songwe.
4. Bw. DENIS BANDISA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya SELESTINE GESIMBA
5. Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Bibi. WAMOJA DICKOLAGWA.
6. Bw. ABDALLAH MOHAMED MALELA ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
7. Bw. RASHID KASSIM MCHATA ameteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Bw. CHARLES PALLANGYO.
8. Bw. MISSAILE MUSSA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Manyara.
9. Bi. CAROLINE ALBERT MTHAPULA ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa MARA.
10. Dkt. JILLY ELIBARIKI MALEKO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya ALFRED LUANDA.
11. Bw. CHRISTOPHER DEREK KADIO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Mstaafu CLODWING MTWEVE.
12. Bw. ERIC SHITINDI ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Njombe. Anachukua nafasi ya BW. JACKSON SAITABAU.
13. Prof. RIZIKI SALAS SHEMDOE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Bw. HASSAN BENDEYEKO.
Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya
kazi.
1. Bibi REHEMA MADENGE aliyekuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa DODOMA, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.
2. Bibi THERESIA MMBANDO aliyekuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa DAR ES SALAAM amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na
Naibu Makatibu Wakuu kwa baadhi ya Wizara kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. JOSEPH
BUCHWESHAIJA kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Anachukua nafasi ya Prof. ELISANTE Ole GABRIEL.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. ANDREW WILSON
MASSAWE kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. ELISANTE Ole
GABRIEL kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo).
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jim James
Yonazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Mawasiliano)
5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. EDWIN PAUL MHEDE
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa
Wilaya na wengine kuhamishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JERRY CORNEL
MURO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. FRANK JAMES
MWAISUMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Anachukua nafasi ya Bw. DANIEL
GEOFREY CHONGOLO.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PATROBAS KATAMBI
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi MWANAHAMISI
ATHUMAN MUKUNDA kuwa Mkuu wa Wilaya ya BAHI. Anachukua nafasi ya ELIZABETH
SIMON KITUNDU.
5. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi
Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido kwenda Wilaya
ya Kinondoni.
6. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bibi SARA MSAFIRI
ALLY aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwenda Wilaya ya Kigamboni. Anachukua
nafasi ya Bw. HASHIM SHAIBU MGANDILWA.
7. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. SAID MKUMBA kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Anachukua nafasi ya JOSEPHAT PAULO MAGANGA
8. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bw. JOSEPHAT
PAULO MAGANGA na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Anachukua nafasi ya HERMAN
CLEMENT KAPUFI.
9. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali PATRICK
NORBERT SONGEA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Anachukua nafasi ya SHAABAN
ATHUMAN NTARAMBE.
10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. RASHID MOHAMED MWAIMU kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa. Anachukua nafasi ya Kanali SHABAN ILANGU LISSU
11. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali SIMON M. ANANGE kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu.
12. Mhe. Rais Magufuli amemteua Luteni Kanali MICHAEL
MASALAMA NGAYALINA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe. Anachukua nafasi ya Brigedia
Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI.
13. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. LENGAI Ole SABAYA kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Hai.
14. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. HASHIM SHAIBU
MGANDILWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa. Anachukua nafasi ya Bw. JOSEPH JOSEPH
MKIRIKITI.
15. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ELIZABETH SIMON
KITUNDU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati. Anachukua nafasi ya RAYMOND HIERONIMI
MUSHI
16. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Hanang. Anachukua nafasi ya SARA MSAFIRI ALLY.
17. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. MARY-PRISKA WINFRED
MAHUNDI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MANASE
MADUSA.
18. Mhe. Rais Magufuli amemteua Ndg. NGOLLO MALENYA kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga. Anachukua nafasi ya Bw. JACOB JOSEPH KASSOMA.
19. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. MOSES JOSEPH MACHALI
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
20. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. SEVERIN MATHIAS
LALIKA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.
21. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILIS MESHACK NYIMBO
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. Anachukua nafasi ya MARY ONESMO TESHA.
22. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILEMON SENGATI kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Magu. Anachukua nafasi ya HADIJA RASHID NYOMBO.
23. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali LUCAS BONIPHACE MAGEMBE
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe. Anachukua nafasi ya ESTOMIH FRANCIS CHANG’AH.
24. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ZAINAB RASHID MFAUME
KAWAWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo. Anachukua nafasi ya Bw. MAJID HEMED
MWANGA.
25. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. JOKATE MWEGELO kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe. Anachukua nafasi ya Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM.
26. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. SOPHIA KIZIGO kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo. Anachukua nafasi ya Bibi. LUCKINESS ADRIAN AMLIMA.
27. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. JASINTA VENANT
MBONEKO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Anachukua nafasi ya JOSEPHINE RABBY
MATIRO.
28. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. RAHABU MWAGISA
SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
29. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PASACAS MURAGIRI kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya ELIAS CHORO JOHN TARIMO.
30. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. KOMANYA ERIC KITWALA
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
31. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. KISA KASONGWA kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Korogwe.
(Orodha imetolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais, IKULU, Dar es Salaam)
0 Comments