Coach Mpya wa Arsenal Unai Emery . |
Unai Emery anajiandaaa kumpa ukapteni Mesut Ozil hii ikiwa ni
Kwa mara nyingine tena baada ya Mshambuliaji huyo Raia wa ujerumani kukiongoza
kikosi hicho kupata ushindi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Paris St Germain
.(London Evening Standard)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema kufungwa mapema
kwa dirisha la usajili Englad hautasaidia klabu, lakini hiyo isiwe sababu ya
kuchanganyikiwa kwa kukosekana kwa wachezaji wapya waliosajiliwa. (London
Evening Standard)
Juventus wanaamini kiungo wa kati Paul
Pogba yuko tayari kurejea kwenye klabu hiyo ya nchini Italia, na wako tayari
kumuuza mshambuliaji Gonzalo Higuain, 30,kiungo wa kati Miralem Pjanic na
walinzi Daniele Rugani, 24, and Mattia Caldara, 24, ili kumgharamia mchezaji
huyo mwenye miaka 25. (Sunday Mirror)
Real Madrid inaelekea kuachana na mpango wake wa kumsaini Eden
Hazard kutoka Chelsea baada ya kukataa bei ya paundi mil 200 aliyowekewa
mchezaji huyo.(Sunday Express)
Chelsea iko tayari kumnyakua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron
Ramsey, kwa kitita cha pauni milioni 30.Aaron amebakisha mwaka mmoja kumaliza
mkataba wake na washika bunduki hao. (Mail on Sunday)
Manchester United inapanga kumnyakua mlinzi wa Barcelona Yerry Mina,23.
(Sun on Sunday)
Borussia Dortmund wanajiandaa kumuuza Christian Pulisic msimu
huu kwa gharama ya pauni milioni 65, Chelsea na Liverpool ni miongoni 'mwa timu
zilizoonyesha nia ya kumchukua.(Mail on Sunday)
liverpool inataka kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi,
kwa pauni milioni 26, lakini Watford wanamtaka mchezaji huyo kwa mkopo
Westham inajiandaa kumnyakua beki wa kati Domagoj Vida kutoka
Besiktas, Monaco nao wakionyesha nia ya kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka
29(Fanatik, via Sunday Express)
Meneja wa Burnley Sean Dyche anataka kumsajili mshambuliaji wa
Stoke City,Peter Crouch, 37, kwa dili la pauni 500,000.(Sun on Sunday)
Everton wamekubali dau la hadi paundi 25 kwa Barcelona Kwa ajili
ya Beki Lucas Digne (25 ) raia wa Ufaransa. (Goal.com)
Arsenal inamlenga Steven Nzonzi, 29, kiungo wa kati wa zamani wa
Blackburn na Stoke ambaye sasa anakipiga Sevilla, yu mbioni kujiunga na Roma
kwa kitita cha zaidi ya pauni milioni 29
0 Comments