MFUGAJI APIGWA FAINI YA ZAIDI YA SHIL MIL 37 SINGIDA


Wafugaji waliyokamatiwa mifugo .
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtavila kata ya Mkilawa Mohamed Rashid Mlangida akifafanua juu ya zoezi zima la kamata kamata hiyo.




Wakazi wa kijiji cha Mtavila wakiongea na waandishi wa habari.




Baada ya waandishi kutishiwa bunduki na Askali  wanyama poli ilibidi kupata picha za n'gombe hao kwa mbali.

Wafugaji wa kijiji cha Mtavila  kata ya Makilawa Wilaya ya Ikungi wameiomba serikali kushugulikia tatizo sugu la tozo ya fainikubwa wanazopigwa bila maelezo ya kutosha kutokana na marisho ya mifugo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Bw Mwabila Gisena mmoja wa wafugaji hao wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kukamatwa mifugo yake zaidi ya n’gombe 670 na kudaiwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 37 kwa kile kinacho daiwa kuingiza katika eneo la hifadhi ya Minyughe iliyopo katika kata hiyo ya Makilawa .

Baada ya kushuhudia mfugaji huyo akilipa faini hiyo bila kuona stakabadhi ya malipo hayo mjini singida jopo la waandishi lilifunga safari zaidi ya kilometa 80 kutoka manispaa ya Singida na kwenda kijiji cha Mtavila ili kuonana na viongozi husika na kufanikiwa kukutana na Mwenyekiti wa kijiji cha Mtavila kata ya makilawa na kufanikiwa  kuzungumza nae.

Chakushanza mmoja wa Askali wa wanayama poli alichukua bunduki na kuanza kukoki huku akitoa maneno makali kwa waandishi wa habari waliyofika kuangalia mifugo hiyo iliyokuwa imefungiwa kwenye zizi kwa zaidi ya siku nne bila malisho wala maji.



Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments