Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (picha ya maktaba)
Mtoto
Mwenge alitupwa chooni na mama yake mzazi Winfrida Lori (23) mwanafunzi katika
Chuo cha Uuguzi cha Kiomboi Wilayani Iramba ambapo mama huyo
amekiri kujifungua mtoto huyo wa kiume katika Kijiji cha Luono Julai 3,
saa mbili usiku kisha kumfunga vitambaa mdomoni na kumtumbukiza chooni.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Kiomboi Regina Alex amesema afya ya Mtoto Mwenge
inaendelea kuimarika pamoja na hali ya mama mzazi wa mtoto huyo pia inaimarika
tofauti na hapo awali ambapo alikuwa dhaifu na kushindwa kumnyonyesha mtoto.
“Winifrida
alikuwa hawezi kumyonyesha mtoto Mwenge hapo mwanzoni lakini sasa hivi
anamnyonyesha vizuri na maziwa yanatoka ya kutosha, Mtoto mwenge ana hali nzuri
na sasa amefikisha uzito wa kilogramu 2.9 hali ambayo inaridhisha kwakweli”,
ameeleza muuguzi huyo.
Muuguzi
Regina ameongeza kuwa licha ya mama wa mtoto Mwenge kuwa chini ya ulinzi wa
jeshi la polisi, ameendelea kumhudumia mtoto wake vizuri na kwa upendo hali
inayosababisha mtoto Mwenge kupata nafuu kwa uharaka.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amempa jina mtoto huyo
la Mwenge amesema kuwa jina hilo litamfutia mtoto huyo majeraha ya kutupwa
chooni na kuwa ishara ya kujiamini, kujipenda, kujithamini na kumpa matumaini
kama ambavyo mwenge wa huru umekuwa ukifanya.
Dkt Nchimbi
amesema mwenge wa uhuru umekuwa ishara ya kuleta matumaini kwa waliokata tamaa,
upendo penye chuki na heshima penye dharau na hivyo kitendo cha mama kumtupa
mtoto ni kukosekana kwa amani, upendo na heshima katika maisha ya mama huyo.
Ameongeza
kuwa anamtakia kila la heri mtoto Mwenge ili atakapokuwa alete heshima, upendo
na amani katika maisha yake na ya wazazi wake huku akifuta kumbukumbu mbaya ya
maisha yake wakati wa kuzaliwa.
Wakati huo
huo Dkt Nchimbi amewaasa wazazi na walezi kuwapa majina mazuri watoto wao
kwakuwa majina huwa ni sehemu muhimu ya maisha ya watoto wao na hutafsiri
maisha ya baadaye.
Dkt. Nchimbi amesema jina linapaswa liwe na maono mazuri kwakuwa
ndio hayo yataambatana katika maisha yake lakini jina lenye baya huleta mambo
mabaya katika maisha ya mtoto.
0 Comments