SINGIDA.
NA
JENESTA ZEDEKIA
Jamii kwa ujumla katika kata ya Ilongero halmashauri ya
Singida walitoa mchango kuhakikisha ujenzi wa zahanati unakamilika kwa wakati
ili kuanza kupata huduma kwa haraka.
Akisoma Risala mbele
ya mkuu wa mkoa wa Singida Afisa mtendaji wa kijiji cha mwahango Bw.Ronald Muna wakati wa
uzinduzi wa zahanati alisema kuwa mradi
huo utasaidia kuinua uchumi pamoja na kipato cha wananchi.
Aidha Bw.Muna alisema mbali na kuinua uchumi kwa wananchi
pia vijiji jirani vitanufaika na mradi huo.
Baada ya risala hiyo mwenyekiti wa halmashairi ya Singida
Bw.Elia Digha akapata nafasi ya kuzungumza huku akimuomba mkuu wa mkoa wa
Singida kuweza kuwa unga mkono kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za waganga.
Naye mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akahitimisha
kwa kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi wa nyumba za wanganga kwa Sh.Laki
Tano na ujenzi unaotarajia kuanzia hivi
karibuni.
0 Comments