Hii
ni baada ya headphone (Hedifoni/kifaa cha kusikilizia sauti kwenye simu na
mitambo mingine ya kompyuta) zilizokuwa zinatumiwa na abiria mmoja kulipuka.
Mwanamke
huyo alikuwa amelala akiwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kutoka Beijing hadi
Melbourne pale alipozinduliwa na mlipuko mkubwa.
Alizitoa
hedifoni hizo, ambazo hutumia betri, upesi kutoka kichwani na akagundua
zilikuwa zinatoa cheche za moto.
Zilishika
moto na kuanza kuyeyuka.
Mlipuko wa headphone
hizo ulimwacha akiwa na masizi usoni pamoja na malengelenge yaliyotokana na
moto kwenye vidole vyake.
Mwanamke
huyo ambaye jina lake limebanwa, ameambia Shirika la Usalama katika Uchukuzi
Australia (ATSB) kwamba alikuwa akilisikiliza muziki mlipuko huo ulipotokea.
"Nilijishika
usoni mara moja jambo lililosababisha hedifoni zangu kujikunja kwenye shingo.
Niliendelea kuchomwa nazo na ndipo nikazishika kwa nguvu na kuzitupa sakafuni.
Zilikuwa zinatoa cheche na kulikuwa na ndimi chache za moto."
Wahudumu walikimbia
na kumsaidia kuzima moto huo kwa kumwagilia hedifoni hizo maji kwa kutumia
ndoo.
Kufikia
wakati huo, betri ya hedifoni hizo pamoja na kifuniko chake cha plastiki
vilikuwa vimeyeyuka na kukwamilia sakafuni.
"Kwa sehemu
iliyosalia ya safari, abiria walilazimika kuvumilia harufu kali ya plastiki
zilizokuwa zimeyeyuka, vipande vya hedifoni hiyo zilivyokuwa vimeungua na
nywele za mwanamke huyo ambazo zilichomeka pia," ATSB walisema kupitia
ripoti baadaye.
Ripoti
hiyo haikusema hedifoni hizo zilikuwa za muundo gani lakini inaaminika kwamba
huenda mlipuko huo ulisababishwa na kasoro kwenye betri za lithium-ion
zinazotumiwa katika hedifoni hizo.
0 Comments