Kapteni Yolanda Kaunda na Lusekelo Mwenifumbo kaunada katikati ndiyo atakuwa kiongozi wa ndege hiyo
|
Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo
|
Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria
kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika
hilo.
Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam
nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .
Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha
ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Ndege hiyo itakuwa
chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa,
Ethiopia.
"Lengo
la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika
uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au
kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines
ilisema.
Ndege
hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.
0 Comments