Mashimo makubwa
yaliyojitokeza ghafla yamemeza barabara yenye njia tano katikati mwa moja ya
miji mikubwa zaidi nchini Japan Jumanne asubuhi.
Kuporomoka kwa barabara hiyo kulianza majira
ya saa kumi na mbili jioni Jumatatu karibu na kituo cha treni cha Hakata ,
kilichopo katika mji wenye shughuli nyingi wa Fukuoka uliopo kusini mwa kisiwa
cha Kyushu.
Mporomoko huo ulianza kwa mashimo mawili
madogo ambayo baadaye yalianza kupanuka hadi kuwa shimo kubwa lenye kina cha
mita 30m na upana wa futi 98.
Hakuna taarifa za majeruhi makubwa, lakini
mifumo ya umeme, maji na gesi ilivurugika katika katika eneo hilo.
Mtangazaji wa kituo cha habari cha NHK aliripoti kuwa mwanamke
mmoja mzee aliteleza kwenye ngazi kutokana giza lililosababishwa na kukatika
kwa umeme eneo hilo.
Shughuli za wahandisi za kupanua zaidi reli ya chini ya ardhi
inadhaniwa kuwa na uhusiano wa mpasuko huo wa ardhi uliosababisha kutokea
ghafla kwa mashimo mapana kwenye barabara, maafisa wa mji wamesema .
0 Comments