Rais mteule wa Marekani Donald Trump
aliyefanya kampeini ya kupinga Bima ya afya inayofaahamika kama Obama care,
sasa amesema atafanyia marekebisho machache kipengee cha sheria juu ya bima
hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu.
Katika mahojiano ya kwanza tangu
achaguliwe rais siku ya Jumanne, Trump ametangaza mageuzi makubwa ya sera punde
atakapochukua nafasi ya Barack Obama katika Ikulu ya White House mwezi Januari
mwaka ujao.
Bwana Trump, aliyesisitiza vikali
kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa mamilioni ya Wamarekani maskini
kupata huduma ya afya kwa bei nafuu punde tu atakapochaguliwa rais, yaonekana
amebadilisha msimamo wake juu ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana
kulegeza msimamo wake juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule
amesema,Clinton ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa.
0 Comments