Mgombea wa urais aliyeshindwa katika uchaguzi
mkuu wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa rais mteule Donald Trump anafaa
kupewa nafasi ili kuongoza.
Akionekana kwa mara ya kwanza tangu kukiri kushindwa ,mgombea huyo wa
chama cha Democrat amesema kuwa ana matumaini kwamba Trump atafanikiwa kuwa
rais wa Wamarekani wote.
''Tumeona kwamba taifa letu limegawanyika sana zaidi ya
nilivyodhania'',alisema bi Clinton.
Donald Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya ushindi mkubwa.
Atafanya mkutano wake wa kwanza wa mpito na rais Obama katika ikulu ya
White House siku ya Alhamisi.
Bwana
Obama alimpongeza mrithi wake katika mazungumzo ya simu mapema asubuhi akisema
kwamba sio siri kwamba yeye na Trump wana tofauti kubwa kati yao.
''Hatahivyo tuko katika timu moja na watu wanafaa kujua kwamba sisi ni
Wamarekani kwanza tunataka taifa hili kuboreka zaidi''.
Bi Clinton aliwaambia wafuasi wake akitaja kushindwa kwake katika
uchaguzi huo katika hotubu yake huko New York.
''Bado hatujaafikia lengo letu .Lakini siku moja mtu ataafikia'',
alisema Bi Clinton.
0 Comments