Hayo yamebainishwa na Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida,Alhaji
Buruhani Mlau kwenye mkutano mkuu wa Bakwata wilaya ya Singida vijijini
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa msikiti wa kati mjini Singida.
Akifafanua zaidi katibu huyo wa Bakwata Mkoa amezitaja sababu zingine
zilizochangia Massaka kusimamishwa kazi kuwa ni ubadhirifu wa shilingi
640,000/=mali ya baraza hilo, kusababisha hasara ya amana ya waislamu wa wilaya
ya Singida vijijini,kudanganya Jumuiya ya Akina mama wilaya ya Singida vijijini
kwa kuchukua gunia moja la mahindi pamoja na kutoonekana hata kidogo mapato
yatokanayo na usajili wa ndoa.
Hata hivyo awali mkutano huo ulipoanza nusura uingie dosari baada ya
mmoja wa wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa,Bwana Jumanne Nkii kutoa maelezo
ambayo hayakuwapendeza wajumbe kutokana na kile walichodai kwamba mjumbe huyo
ni moja ya watu wanaoihujumu Halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.
Wakichangia maelezo ya wajumbe kutoka Bakwata Mkoa baadhi ya wajumbe
wa wilaya,Bwana Issah Mwiru ametaka kufahamu sababu zilizowafanya wao
waitwe kwenye mkutano huo wakati walishakamilisha maamuzi yao ya kutokuwa na
imani na mtendaji huyo na kufikia maamuzi ya kumsimamisha kazi.
0 Comments