Pep Guardiola amesema hatabadili
Falsafa ya Mbinu zake licha ya Manchester City Jana kutwangwa 4-0 na Klabuyake
ya zamani Barcelona huko Nou Camp kwenye Mechi ya Kundi C la UCL, UEFA
CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi hiyo Lionel Messi
alipiga Hetitriki na moja kufungwa na Neymar huku Kipa wa City Claudio Bravo,
Mchezaji wa zamani wa Barca, aliefanya kosa kubwa na kuzawadiwa Kadi Nyekundu
katika Dakika ya 54.
Guardiola ameeleza: “Hamna
mabadiliko. Mpaka Siku yangu ya mwisho kama Kocha ntajaribu kuanza kwa kucheza
toka kwa Kipa wetu!
Huku Barca wakiongoza Bao 1, mapema
Kipindi cha Pili, Kipa Bravo aliinasa Pasi ndefu na alipotaka kuanza Mpira kwa
Beki wake kama ilivyo kawaida yake badala ya kupiga mbele, Pasi yake hiyo
ikanaswa na Luis Suarez ambae alipiga juu Mpira kumvuka Bravo na Kipa huyo
akaruka juu na kuucheza Mpira kwa Mikono wakati akiwa nje ya Boksi.
Kwa kosa hilo, Bravo akapewa Kadi
Nyekundu na City kubaki Mtu 10
Kuhusu kosa hilo la Bravo ambae
aliletwa City kutoka Barca kumbadili Kipa Namba Wani wa England Joe Hart kwa
sababu tu hutumia miguu kuanzisha Gemu toka Golini na kuwapasia Mabeki wake
badala ya kubutua mbele, Guardiola ameeleza: “Wakati mwingine kuna makossa ana
wakati mwingine unalazimika kupiga Mpira nje lakini mara nyingi, tukicheza
vizuri, Mpira huanzia kwa Pasi ya Kipa.”
Aliongeza: “Ni wazi anajua
alichofanya kwa sababu ana uzoefu mkubwa nay eye ni mmoja kati ya Makipa Bora
katika Miaka 10 iliyopita, sina wasiwasi nae!”
Hivi sasa City hawajashinda katika
Mechi zao 4 zilizopita lakini bado wapo kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, na
kipigo hiki ni cha kwanza kwa Guardiola katika Mechi zake 11 tangu ashike
hatamu Msimu huu.
0 Comments