Dar -es-Salaam
Na Mwandishi wetu
Tarehe 20 Novemba,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, aliwatembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa
lililotokea Kariakoo, Jijini Dar es Salaam. Majeruhi hao wamelazwa katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala.
Katika ziara
hiyo, Rais Samia aliwajulia hali na kuwafariji waliopatwa na majeraha, huku
akiwapa pole kwa msiba na changamoto waliokumbana nazo kutokana na ajali hiyo.
Pia alitoa wito wa mshikamano na msaada wa haraka kwa wahanga wa tukio hilo,
akisisitiza dhamira ya serikali katika kushughulikia majanga kama haya kwa
ufanisi zaidi.
0 Comments