VIONGOZI WA UWT KUWAHIMIZA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO SHULE.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake UWT Mkoa wa Singida Martha Kayaga akiongea na Wanachama UWT wa Wilaya ya Iramba ikiwa nikatika Ziara ya Kukagua na kuongea na wWanawake wa Iramba.

Grace Mkoma Mjumbe wa Baraza UWT Taifa akitoa Elimu kwa kinamama wa Wilaya ya Iramba juu ya upatiakanajio wa Mikopo  kupita Vikundi vya Kinamama.

Mwenyekiti wa Jumuiya Wanawake Mkoa wa Singida Martha Kayaga akisisitiza Jambo juu ya kujiandikisha katika Daftari la Mkazi.


Picha ya Juu Mweyekiti wa UWT Mkoa Martha Kayaga akisaini kitabi cha wageni na Picha ya chini Mbaraza UWT Taifa Grece Mkoma pia akisaini Katika Kitabu Cha Wageni Wilayani Iramba.

 Katikati ni Mwenyekii wa UWT Mkoa wa Singida Martha Kayaga Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba na Kulia ni Katibu wa UWT Mkoa wa Singida.



Katibu wa UWT Wilaya ya Iramba Judith Laizer akitoa taarifa ya Wilaya kwa Mwenyekiti wa Wilaya na Kamati ya Utekelezaji 



Viongozi wanawake wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mzazi ama mlezi anampeleka mtoto wake shule ili mtoto apate haki yake ya msingi katika maisha yake kwani Serikali imeboresha miundombinu katika sekta hiyo.

 

Mwenyekiti wa jumuiya ya UWT CCM Mkoa wa Singida Martha Kayaga ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wanachama na Viongozi wa jumuiya hiyo Wilaya ya Iramba katika ziara kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo ya kuhamasisha wananchi hasa wanawake kujitokeza kugombea na kushiriki kikamilifu katika chaguzi zijazo.

Amewaambia wanawake hao kuwa mwanamke yeyote ni kiongozi hivyo wanapaswa kutoa ushirikiano wa kuhamasisha kila mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto wake shule.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi za UWT Wilaya,katibu wa jumuiya hiyo Wilaya ya Iramba Judith Laiza amesema hali ya siasa katika Wilaya hiyo ni shwari.

 

Kwa upande wake mwakilishi wa jumuiya hiyo taifa akitokea Mkoa wa Singida Grace Mkoma amewataka na kuwahamasisha wanawake wajasiriamali kuunda na kusajili vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali kwa lengo la kuinua vipato vya wananchi.

 

Ziara ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi UWT Mkoa wa Singida inatarajiwa kufanyika Wilaya zote ambapo lengo ni kuhamasisha wanawake kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments