Kocha Mkuu wa Timu ya Ihefu Fc Mecky Mexime akiongea na wanahabari Baada ya mchezo wa Kombe la CRDB FERDERATION CUP kumalizika dhidi ya Mashujaa Fc na kupata ushindi kwa njia ya Mikwaju ya Penalti
WAPENZI wa soka mkoani Singida wameombwa kutambua kuwa timu ya
soka ya Ihefu,ni timu yao hivyo wanapaswa kuisapoti zaidi, ili iweze kuendelea
kufanya vizuri kwenye ligi mbali mbali.
Wito huo umetolewa juzi na kocha mkuu wa Ihefu,Mecky Mexine muda
mfupi baada ya kuitoa nje timu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma, kwenye ligi ya
kombe la CRDB Bank Federation .Kwa mikwaju ya penalty.
“Wana Singida hii Ihefu ni yenu wakiwemo na Wanyiramba. Msiiache
kabisa kuisapoti kwa hali na mali.Ndugu zangu njooni….bila ninyi hatuwezi
kabisa kwenda.Siogopi,mkiwepo na ari kwa wachezaji,inaongezeka
zaidi”,amehimiza.
Amesisitiza zaidi kwamba mashindano hayo ni makumbwa (ni ya
kimataifa),na yanaendelea bado… hatua moja mbele, yatahamia ngazi ya kimataifa.
Hata hivyo,mkongwe Maxime amewapongeza sana wapenzi wa soka
waliojitokeza kuisapoti timu yao juzi, na kutoa sapoti iliyochangia Ihefu
waweze kuwachapa wageni wao.
Dalili zilianza kuonyesha mapema kuwa Ihefu inaweza kuibuka na
ushindi,baada ya kumiliki kipindi chote cha kwanza kwa kuliandama lango la
wapinzani wao.
Hata hivyo wafungaji hawakuwa na utulivu pindi wanapolifikia
lango la wenyeji wao.Wageni mashujaa wao walikimiliki kipindi cha pili
mwishoni,na shida ni ile ile inafanana na ya Ihefu,umakini haukuwepo.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Mashujaa,Abdala Mohammed,ametumia
fursa hiyo kumshukru Mungu,kwa kumalizika salama mchezo huo ulikokuwa na
ushindani mkubwa, hasa kipindi cha pili.
“Tumepoteza nafasi nyingi za kufunga hasa kipindi cha pili.Hali
hii imechangia tuingie kwenye matuta ambayo kwa upande wetu,yametugharimu.Kwa
ujumla hii ni ziara…..sasa tunafokasi kwenye ligi kuu”,amesema huku akionyesha
wazi amesikitishwa na matokeo ya mchezo.
Mkazi wa tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi,Isekuu
Nathaniel,amemshauri Maxime mapema aangalie uwezekano wa kuipa jina jipya timu
ya Ihefu (hili la Ihefu,halieleweki)Jina hilo jipya liwe na angalau harufu ya
Kinyiramba,kinyaturu au hata la kisukuma wale wa wilaya ya Manyoni.
Amesema sio tu jina,viongozi waangalie uwezekano wa kuanzisha
timu za viwango mbali mbali kila wilaya,ili kupata vijana wa mkoa huu, ambao
watatangaza vema mkoa.
Tofauti na sasa ambapo timu zinaitwa majina ya Singida,lakini
hakula hata mzawa mmoja ndani ya timu husika.Wote ni wa kuja na hivyo hawana
kabisa mapezi ya kweli na mkoa wa Singida.
Katika hatua nyingine, meneja biashara wa kanda ya
kati,CRDB benki ,Andrew Mheziwa,alisema kuanzia sasa wataanza
kuhamasisha wananchi kupenda michezo ukiwemo wa soka kupitia CRDB.
“Kuanzia juzi tumeanza kutoa zaidi kwa mchezaji bora wa siku
kwenye mchezo kati ya Ihefu na Mashujaa FC.Juzi tumemzawadi mchezaji bora Jeash
Onyango wa Ihefu shilingi 500,000.Kiasi hicho cha fedha,kitapitia kwenye
akaunti ambayo itakuwa CRDB.Lengo tunataka kukuza michezo kupitia
benki yetu”,amefafanua.
0 Comments