MWAMUZI WA KWANZA MWEUSI KUCHEZESHA EPL.

                                                                Hickson Lovence

Tarehe 26 Disemba, Sam Allison atakuwa mwamuzi wa kwanza mweusi kuchukua jukumu la kuchezesha mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza ndani ya miaka 15 - Sheffield United itakapo kabiliana na Luton Town.

"Nadhani ni mafanikio makubwa, lakini bado kuna safari ndefu," mwamuzi Hickson-Lovence ameiambia BBC Sport.

Allison (42), aliyekuwa afisa wa zimamoto - ameteuliwa kwenye kikosi cha Professional Game Match Officials Limited (PGMOL), ambayo imejiwekea malengo ya kuongeza utofauti wa maafisa wa mechi za soka.

Baraza tawala linataka kuongezwa kwa waamuzi 1,000 wanawake na waamuzi 1,000 weusi au Waasia katika viwango vyote vya ligi katika kipindi cha miaka mitatu.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments