Mtibwa Suger |
Timu ya wakatamiwa ya Tuliani mji kasoro bahari Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3 -0 dhidi ya Singida united katika dimba la Namfua.
Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi 30 baada ya
kucheza mechi 21 na kuendelea kukamata nafasi ya sita, nyuma ya Singida United
yenye pointi 36 kufuatia kucheza mechi 33.
Mabao ya Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani,
Zuberi Katwila yamefungwa na Kelvin Sabato, Salum Kihimbwa na Hassan Dilunga.
Sabato alifunga bao la kwanza dakika ya 21 kwa shuti la mpira wa
adhabu lililotinga nyavuni moja kwa moja, kabla ya Khimbwa kufunga la pili
dakika ya 53 akimalizia pasi nzuri ya Dilunga, ambaye naye alifunga bao la tatu
dakika ya 71 kwa penalti.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki Roland Msonjo wa Singida
United ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm, kumchezea rafu kiungo Salum
Kihimbwa kwenye eneo la hatari.
Katika mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbao FC imelazimishwa
sare ya 0-0 na Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Kwa sare hiyo, Mbao FC inabaki kwenye eneo la hatari ya kushuka
daraja, ikifikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 23 na kuendelea kukamata
nafasi ya 14 katika ligi ya timu 16, mbele ya Njombe Mji FC yenye pointi 18 za
mechi 22 na Maji Maji FC pointi 16 za mechi 22.
Lipuli FC inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 23 na
kuendelea kukamata nafasi ya saba, ikiwa juu ya Mbeya City na Ruvu Shooting ya
Pwani zenye pointi 25 kila moja baada ya kucheza mechi 22 pia.
0 Comments