MGOGORO wa Ardhi ya Shule ya Msingi Mnang’ana Kata ya Sepuka
Wilaya ya Ikungi mkoani Singida uliodumu kwa miaka minne (4) kwa kushtakiana na
mahakakamani kati ya viongozi na wananchi umemalizika juzi baada ya serikali kuamua
kuyapima upya maeneo yote ya shule hiyo na sehemu inayobaki wananchi
wakabidhiwe.
Katika mkutano wa hadhara juzi kijijini hapo maamuzi ya mgogoro
huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungu Miraji Mtaturu amesema Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa alifika hapo kuangalia kati ya viongozi wa
kijiji, uongozi wa shule na wananchi wana matatizo gani.
“Mtaturu amewataka viongozi wa serikali za vijiji kuwatumia
wazee inapotokea matatizo kama haya kwenye maeneo yao ya migogoro ya ardhi
ndipo maamuzi mengine yafanyike na hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa
ugomvi kati ya viongozi wenyewe na wananchi” Alisema.
Taarifa aliyoipewa Mkuu wa Wilaya na Afisa Ardhi juu ya mipango
ya shule ina ekari 94.6 lakini kijiji kiliambiwa maeneo ya shule ni ekari 66
hapo mgogoro ukaanza ikabidi serikali kuyapima upya maeneo ya shule ili
kujiridhisha.
Mtaturu aliendelea kusema maamuzi ya serikali kwa nia moja
maeneo yote ya shule yalindwe, yaheshimiwe na yasivamiwe na watu ovyo ovyo
yaachwe wazi kwa matumizi ya shule tu, hivyo mahusiano yaliyoharibika kijijini
yarejee upya watu wasonge mbele katika kujiletea maendeleo.
Mtaturu amedokeza kuwa matatizo ya kijiji hicho siyo maeneo ya
shule na mipaka yake ni mali yao bali ni chuki binafsi kwani shule ilipanda
miti 137 na mikorosho 50 ikang’olewa yote shule na serikali iliotoa miti
hiyo ikapata hasara sasa waliyoing’oa wanaugomvi na serikali au wanaugpmvi na
viongozi wa shule. Aliuliza.
Miti hiyo ilitolewa na serikali kwa gharama kubwa na ikapewa
shule nayo tangu mwaka 2015 shule ingeanza kupata mapato siyo sahihi kung’oa
miti akatoa mfano, “unapogombana na mwenye nyumba mbwa wake unampigia nini?”
“Sisi sote tukubali kulitokea makosa tangu mwanzo juu ya mipaka
ya shule hii lakini sasa serikali imeliona hilo na serikali itapima upya eneo
lote la shule zipatikane ekari 50 zinatosha kwa majengo yote ya shule
yaliyobaki na zinazobaki viongozi wa serikali ya kijiji na wananchi watakaa,
wataamua watazitumiaje.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Hamisi Abdalaah Mwangu
amesema serikali katika kutatua mgogoro huo ilimtuma Afisa Ardhi kuweka bikoni
kama alama ya mipaka ya shule na iliwekwa lakini baadhi ya wananchi wa kijiji
hicho hawakukubali wa kuondoa moja wakavamia maeneo ya shule wakalima na
kuchungisha mifugo.
Mwanga amesema hapo uongozi ukaanza kati ya uongozi wa shule na
wananchi hao na viongozi wa kijiji wakafuata maagizo ya serikali mgogoro mkali
ukaibuka ukafikia hatua mbaya mpaka kuchafua viongozi, viongozi wakawa wanalala
na viatu wakihofia maisha yao lakini sasa maamuzi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa
Mtaturu yameleta amani kwa watu wote kijijini.
Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Isack Mtinda
amesema mgogoro wa shule yake sasa umeisha na kazi waliyonayo sasa ni kuchapa
kazi, waliyopewa na taifa ili watoto wa wazazi wa kijiji cha mnang’ana wapate
elimu.




0 Comments