TASAF IKUNGI WAPONGEZA KUJENGEWA BWAWA ,BARABARA

 


MRADI wa kunusuru kaya maskini nchini TASAF wilayani Ikungi umeweka mpango mkakati kuhakikisha kaya maskini zinafikia hatua kubwa kiuchumi kwa kuwashirikisha walengwa ujenzi wa bwawa na barabara ndogo vijijini na kazi zingine ndogondogo muhimu kwenye maeneo yao kulingana na maelekezo ya viongozi wao.

Katika kuitikia wito huo kikundi cha watu 133 na viongozi wao walioandikishwa kwenye mradi wa TASAF ya nguvu kazi Kijiji cha Msungua Kata ya Sepuka wilayani Ikungi Mkoa wa Singida wamejenga bwawa kubwa la kufugia samaki na kunwesha mifugo yao wakati wa kiangazi na wametengebeza barabara km 6. Inayounganisha vijiji kwa nguvu zao kwa siku tisini.

Wanatasafu hao wamepongezana kwa kufanya sherehe ndogo baada ya kukamilisha kazi walizopewa utengenezaji wa barabara km6 na bwawa baada ya kuchoshwa na ukosefu wa usafiri na usafirishaji wa mazao yao kwenye soko kuu mjini Singida kwa mauzo.

Katika barabara hiyo kulikuwepo na vichaka, magogo, vigogo, maji na tope hasa vipindi vya masika wanafunzi hao walikuwa wanapata taabu kuvuka, mbuga yenye maji na tope kwenda shuleni katika hali hiyo wanatasaf waliamua waitengeneze barabara hiyo ya kilomita 6 kutoka ofisi ya Kijiji hadi Nyeghee kwa kwa kuondoa vichaka, magogo na maji pamoja na kuipanua ili magari mawili yapishane.

Barabara hiyo itahamisha wananchi inamopita barabara hiyo kulima mazao mikakati katika kujiletea maendeleo na wao kupata usafiri na wanafunzi kufika shuleni bila kuchelewa na sasa wanaimba Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wafanye utaratibu barabara hiyo sasa iwape TARURA wasaidie ujenzi wake.

Diwani wa kata ya Sepuka Halima Ng’imba amewapongeza wanatasafu wa Kijiji cha Msungua kwa hatua walioifikia na hiyo ndiyo dira ya Chama cha Mapinduzi wananchi kwenda na kasi anayotaka Rais wao amewataka wanatasaf hao watakapopata malipo yao ya siku tisini  wayatumie vizuri yalete mafanikio kwao na kwa jamii.

Halima amesema barabara hiyo inaunganisha vijiji vitatu Msungua, Irisya na Uhamaka na itarahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na wao wenyewe kupata usafiri na wanafunzi kupata urahisi wa kwenda shuleni bila woga pia akina mama wajawazito na Watoto kusafiri hadi vituo vya huduma za kiafya kupata chanjo na tiba.

Kaimu Mratibu wa TASAF wilaya ya Ikungi James Masolwa amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi inawapongeza sana wananchi wa Kijiji cha Msungua kwa kuonyesha maendeleo mazuri kwa ujenzi wa bwawa na barabara itakayowaletea maendeleo.

Msolwa amesema maana ya serikali ya Mama Samia kuanzisha mfuko huo wa TASAF  ni kuokoa na kunusuru kaya maskini nchini ili kuondokana na umaskini hivyo walengwa watumie fedha watakazopata kusomesha Watoto wao na kuweka akiba na kupata huduma za msingi kutokana na  mfuko huo.

Aidha Afisa Mtendaji wa Kata ya Sepuka Abella Kibanda amedokeza mradi huo ukiisha uache mafanikio Kata ya Sepuka kwa kuwaletea wananchi maendeleo makubwa kwa kupunguza umaskini ndani ya jamii na itakuwa vizuri kama barabara hiyo itaingizwa TARURA ili iweze kujengwa vizuri ili itumike muda wote.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho Abdallah Jingi, Elifuraha Ambarangu, Juma Hango, Missai Senge na Hassani Megheko wamesema ni vema barabara hiyo iandikishwe TARURA, ipanuliwe vizuri sehemu korofi ili wanakijiji wasafiri wao wenyewe na kusafirisha mazo wanayolima.

Mwisho.  

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments