UKABILA HAUNA NAFASI, TUJENGE TAIFA - KINANA

 



 Makamu  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) BaraComred Kinana akiongea na viongozi wa chama cha Mapinduzi katika ukumbi wa mikutano  wa ofisi za CCM Mkoa wa Mara Musoma Mjini.
    
    Comred Abdulrahaman Kinana akiweka mauwa kwenye kaburi la baba wa taifa Butiama.

Comred Kinana akiongea na Mtoto wa Baba wa Taifa Madaraka Nyerere Butiama nyumbani kwa hayati Mwl Julias Kambarage Nyerere.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amewasisitiza wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuachana na tabia za ukabila akieleza kuwa ni mambo ya kizamani na yanawagawa.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Kinana leo Aprili 15, 2024 mjini Shirati wilani Rorya, amesema nchi kuwa na makabila ni jambo la kawaida ila ukabila ni jambo baya, lisilopaswa kupewa nafasi.

Kinana amesema hayo baada ya baadhi ya wajumbe kuibua hoja kwamba kuna mambo yanafanyika katika wilaya ya Roria ambayo yanaashiria kuwepo kwa changamoto ya ukabila miongoni mwao.

Ameeleza kwamba Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ametoka mkoani humo, kutoka kabila dogo, lakini ameongoza nchi kwa miaka 24, na kwamba alipendwa, aliheshimiwa na kuthaminiwa.


"Sasa usimpe mtu nafasi ya uongozi kwa sababu ya kabila lake, dini au umbile usimuhukumu, hayo ni mambo ya kizamani sana, tuangalie mtu anauwezo atafanya kazi atajituma na kujitolea, mnampima kwa vigezo sio kwamba huyu ni ndugu yangu.


Katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti Kinana amefika Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo alizuuru kaburi lake na kuweka shada la maua.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments