Afrisa Mkuu wa Biashara wa betPawa Ntoudi Mouyelo akizungumza katika hafla ya kutangaza udhamini wa timu za taifa za mpira wa kikapu za Uganda wenye dhamani y ash bilioni 2.6 za Uganda sawa na sh1.8 bilioni za Tanzania.
Afisa Mkuu wa Chapa (Brand) wa betPawa, Spencer Okach, akizungumza katika hafla ya kutangaza udhamini wa timu za taifa za mpira wa kikapu za Uganda wenye dhamani y ash bilioni 2.6 za Uganda sawa na sh1.8 bilioni za Tanzania.
Waziri wa michezo wa Uganda Peter Ogwang akizungumza katika hafla ya udhamini wa timu za taifa ya mpira wa kikapu.
Katibu Mkuu wa baraza la michezo la Uganda Bernard Ogwe akizungumza katika hafla ya udhamini wa timu za taifa za mpira wa kikapu.
Maafisa wa kamati ya timu za Taifa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Uganda (FUBA), watendaji wa betPawa na wawakilishi wa timu mbili za kitaifa za mpira wa kikapu za wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya sherehe ya kusaini mkataba wa udhamini.
Timu za taifa za mpira wa kikapu za wanaume (Silverbacks) na wanawake (Gazelles)
zimepata udhamini mnono kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa wenye
thamani ya sh2.6 bilioni za Uganda, sawa n ash Bilioni 1.8 za Kitanzania.
Mkataba wa udhamini huo wa miaka mitatu ulisainiwa jana kati
ya maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Uganda (FUBA) na viongozi wa
ngazi za juu wa betPawa.
Mbali ya kugharimia timu hiyo katika michezo mbalimbali ya
kimataifa, betPawa pia itagharimia kambi ya timu, usafiri, malazi, gharama za
kushiriki katika mashindano mbalimbali, bifa ya afya na mambo mengine muhimu za
timu hizo.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Afisa
Mkuu wa Chapa wa betPawa, Spencer Okach alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa
kuchangia maendeleo ya michezo nchini Uganda.
"Lengo letu ni kuhakikisha Uganda inapata
maendeleo makubwa katika mpira wa kikapu na michezo kwa ujumla ndiyo maana
tumeingia mkataba mkubwa wa udhamini,” alisema Okach.
Alisema kuwa kupitia udhamini huo, betPawa pia italipa
moja kwa moja kiasi cha Sh150,000 za Uganda (Sh98,000) za Tanzania kama bonasi
ya ushindi kwa kila mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda. Bonasi hiyo ni kwa
ushindi kwa mechi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa FUBA, Marcus
Kwikiriza aliipongeza kampuni ya betPawa kwa udhamini huo mnono kwani umeweka
historia.
"Hii ni mara ya kwanza wachezaji wetu wanapata
motisha ambapo kampuni binafsi ya betPawa inadhamini timu ya kitaifa
ya mpira wa kikapu,” alisema Kwikiriza.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Idara ya Michezo wa
Uganda, Peter Ogwang alipongeza betPawa kwa udhamini huo akibainisha kuwa
katika nchi nyingi michezo inasaidiwa zaidi na sekta binafsi.
Ogwang alisema kuwa anatarajia timu hizo za taifa kufanya
vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
"Ni faraja kubwa na wadhamini wanastahili pongezi
kubwa. Matatizo yanayokabili michezo yanaweza kutatuliwa tu na washirika
tulionao hapa. Mahali pengine, wadhamini binafsi wanakuwa na jukumu kubwa
katika kusaidia timu. Asante kwa betPawa kwa kuleta changamoto hapa," alisema.
Naye Meneja na msimamizi wa timu hizo, Albert Ahabwe
alisema maendeleo ya timu zao awali yaliathiriwa na matatizo ya
kifedha pamoja na kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa betPawa, Ntoudi
Mouyelo alisema kuwa kampuni yao ina mipango mikubwa ikiwa pamoja na kuwa ya
kwanza barani Afrika.
Mouyelo alisema udhamini wao umekuwa wa wakati muafaka
kutokana maendeleo makubwa ya mpira wa kikapu na Ligi ya Mpira wa Kikapu ya
Afrika (BAL).
Alisema ushirikiano wao na FUBA utaleta maendeleo chanya
ya mchezo huo hasa kwa wachezaji na klabu kwani betPawa itawawezesha
kushindana katika michezo mbalimbali.
“Timu ya wanaume (Silverbacks) imetajwa na Shirikisho la
mpira wa kikapu duniani (FIBA) kuwa moja ya timu ambayo imepanda katika viwango
kwa nafasi nne mpaka kufikia ya 83 kati ya nchi 160. Haya ni maendeleo makubwa,
udhamini wetu huu utasaidia kupanda chati zaidi duniani,” alisema.
0 Comments