UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA JIMBO LA MH MARY NAGU WAANZA RASIMI

Mh Merry Nagu akishiriki katika zoezi hilo la ujenzi Kitongoji cha Kinachere,kata ya Sirop,tarafa ya Simbay,wilayani Hanang,Mkoani Manyara




Na,Jumbe Ismailly HANANG 

WANANCHI  300 wa Kitongoji cha Kinachere,kata ya Sirop,tarafa ya Simbay,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Hanang wameanza ujenzi wa kisima na tenki la kuhifadhia maji ya mvua lililopo juu ya jiwe ili waweze kuondokana na adha ya kufuata huduma hiyo  umbali wa zaidi ya mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji hicho,Bwana Peter Qwendo(Kwendo) amesema mradi huo utakapokamilika unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi milioni 49 na kwamba kati ya kiasi hicho cha fedha asilimia kumi ya gharama za mradi huo ni mchango wa wananchi kwa kufanyakazi ya kukusanya mawe,mchanga,kokoto,kuchota maji na kumwagilia.


Aidha Qwendo (Kwendo) ambaye pia ni mmoja wa watu waliokwenda Nchini Kenya kupata mafunzo juu ya usimamizi wa shughuli hiyo,amesema wananchi hao wanaoishi katika kaya 107 wamekuwa wakiifuata huduma hiyo katika Kitongoji cha Ghata kilichopo umbali wa takribani kilomita 14 kwenda na kurudi.


Kwa upande wake Msimamizi wa Mpango wa afya wa Kijiji cha Nangwa,Bwana Apolei Wilbrod ameweka bayana kwamba wafadhili wa mradi huo ni Medical Missionary Of Mary Nangwa wanaoendesha huduma za Kliniki ya mama na mtoto katika wilaya ya Hanang.  Kwa mujibu wa Wilbrod kabla ya kuanza kwa mradi huo wa tano,shirika hilo lisilokuwa la kiserikali lilianzisha miradi mingine ya aina nne mwaka 2014 na kwamba madhumuni yake yalikuwa kuwasaidia wananchi waliopo kwenye maeneo hayo na kwamba unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja na utagharimu jumla ya shilingi milioni 49,700,000/=.


Hata hivyo Msimamizi huyo wa mradi ametumia pia wasaa huo kutoa wito kwa wadau wengine kujenga utamaduni wa kushirikiana wakati wote na jamii kwa kufurahia miradi husika ili iweze kuwasaidia wananchi.


Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu aliyetembelea mradi huo kwenye ziara yake inayoendelea katika jimbo hilo amebainisha kuwa utaratibu mzuri waliojiwekea ni kwamba wananchi wanalazimika kuchangia asilimia kumi na Halmashauri asilimia kumi ya mradi huo ambapo hata hivyo ameahidi kuwapatia malori matano ya mchanga.




Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments