Joel Bendela mkuu wa mkoa wa manyara akiongea katika mafunzo hayo pembeni ni Mgeni rasimi mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi |
Imeelezwa kuwa lengo la baraza la uwezeshaji wananchi Tanzania ni kuhakikisha wananchi wanashiriki ipasavyo katika suala zima la kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi taifa Dr,John Jingu wakati wa mafunzo ya uwezeshaji yaliyo wakutanisha wakuu wa mikoa ya kanda ya kati, Geita na Shinyanga, wakuu wa wilaya pamoja na maafisa mipango wa halmashauri na mikoa.
Amesema ili malengo ya baraza hilo yakamilike ni lazima kila kiongozi kwenye eneo lake kuwajibika kwa kushirikiana na wananchi ili kuinua uchumi katika eneo hilo
Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Singida Dr, Rehema Nchimbi amewaomba viongozi kuyatumia ipasavyo mafunzo hayo ili kuinua uchumi kwa wananchi.
Dr,Rehema amesema kuwa mafunzo hayo yawe chachu ya kuhakikisha adhima ya Serikali ya unchumi wa kati na nchi ya viwanda inatimia ifikapo mwaka 2025
0 Comments