Bingwa
mtetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika, USM Alger ya Algeria imegoma kuingiza
timu kwenye Uwanja wa Berkane Municipal kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya
pili ya michuano hiyo dhidi ya RS Berkane ya Morocco, uliopangwa kupigwa saa
4:00 usiku.
USM Alger ilifika hadi kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo lakini hawakuingia uwanjani na badala yake wameondoka na
kuwaacha wenyeji Berkane.
Iko hivi, mchezo wa nusu fainali ya kwanza
ulishindwa kufanyika baada ya wageni Berkane kuzikataa jezi walizozikuta kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo wakidai sio zao.
Awali, RS Berkane ilidai jezi zao zilizuiwa Uwanja
wa Ndege walipowasili Algeria kisha wakawaambia hawataruhusiwa kuzitumia kwa
kuwa zina Bendera ya Morocco, jambo lililopingwa na timu hiyo, wakidai wanataka
kuzitumia na ikishindikana hawataingiza timu uwanjani, jambo ambalo lilitokea.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilifanya uamuzi
wa kuipa ushindi RS Berkane wa alama tatu na mabao 3-0 baada ya kubaini
Wamorocco hao walifanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na wenyeji wao USM
Alger.





0 Comments