TAKUKURU SINGIDA YAOKOA ZAIDI YA MIL 28, MIRADI YA MAENDELEO.

 Mkuu Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake Singida Mjini.






Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Singida imeokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 28 kwenye miradi 5 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 iliyokuwa ikitekelezwa mkoani humo. 

Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida Sipha Mwanjelwa ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya utendaji kazi wa kipindi cha januari hadi machi mwaka huu.

 

Amesema Kufuatia ufuatiliaji uliofanywa na TAKUKURU kwa kipindi hicho miradi 5 ilikutwa ina mapungufu ikiwemo kufanya malipo ya vifaa vya ujenzi kwa wazabuni yanayohusisha gharama ya Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) wakati wazabuni hao hawajasajiliwa kwenye mfumo huo.

 

Hata hivyo Mkuu huyo amesema kwa robo ya nne ya kuanzia mwezi aprili hadi juni mwaka huu TAKUKURU imeweka mikakati ya utendaji kazi,huku akitoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa na kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo hivyo.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments