MADHARA YA MFUMO JUMUISHI NI TATIZO NCHINI.

 

         Hakimu Mkazi Mfawidhi Alu Nzowa akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama ya Mkoa wa Singida.

Shekh Mkuu wa Mkoa wa Singida Issa Nassor akitoa maoni yake juu ya malekebisho ya Sheria ya kifo na ufafanuzi wake katika baadhi ya vipengele sambamba na maoni yake wakati akiongea na waandishi wa Habari.



             Mahakim wa mahakama ngazi mbalimbali kutoa mkoa wa Singida wakisiliza hotuba za vingozi.


Wakili Msomi Cosmas Luambao  Rais wa chama cha Mawakili wa kujitegemea (Tanganyika Law Society -TLS) Mkoa wa Singida akitoa taarifa ya Mawakili.


                        Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa Singida Yusuph Mhoja Kasuka akifanya utambulisho

Jaji Mstaafu Fatuma Masenga akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragiri.



Watumishi wa Mahakama


                                               picha ya kumbukumbu na watumishi wa mahakama

Imeelezwa kuwa maboresho ya kimkakati katika tasnia ya utoaji haki yanatakiwa kuwa jumuishi katika kuboresha sera, sheria, kanuni na mfumo wa makosa jinai nchini kwa maendeleo na ustawi wa Taifa.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Mkoa wa Singida Alu Nzowa ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki na siku ya sheria nchini Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya mkoa.

Hakimu Nzoa amesema maendeleo na ustawi wa Taifa yanategemea uwepo wa usalama, amani na utulivu ambapo vitu hivyo vinahitaji zaidi kuwepo kwa haki katika jami

Katika hatua nyingine hakimu Nzoa ameeleza kuwa madhara ya kutokuwa na mfumo jumuishi wa haki jinai unasababisha ucheleweshaji wa haki,wadau kuchukua muda mwingi na rasilimali katika kuendesha mashauri mahakamani.

Aidha sheikh mkuu wa Mkoa wa Singida Isa Nassoro Isa ametoa wito kwa mahakimu kutenda haki ili jamii iwe na amani pia ametumia nafasi hiyo kuwashauri wanasheria na mawakili wa kujitegemea kuisaidia jamii kupata haki na sio kutanguliza mbele maslahi yao binafsi.


 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments