Shirikisho
la Soka la Kimataifa FIFA na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeifungia
klabu ya Yanga kusajili wachezaji wa kimataifa na wa ndani.
Mashirikisho hayo yamefikia uamuzi huo baada ya
aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Lazarus Kambole kushinda kesi ya madai dhidi ya
klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na TFF
imesema Kambole aliishitaki Yanga kwa madai ya malimbikizo ya mshahara na fidia
ya kuvunjiwa mkataba, ambapo timu hiyo ilipewa siku 45 kulipa pesa hizo na
ilishindwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kushindwa kutekeleza
hukumu ndani ya muda husika ndio sababu ya timu hiyo kufungiwa kusajili usajili
wa ndani na wa nje.
Yanga ilimtambulisha Kambole raia wa Zambia Juni
16, 2022 akitokea Kaizer Chiefs ambapo Septemba,2022 iliachana na mchezaji huyo
na kumpeleka kwa mkopo kwenye timu ya Wakiso Giant ya Uganda.
0 Comments