Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe akiongea katika maziko hayo mbele ya familia na ndugu na jamaa wa marehemu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe ameshiriki katika shughuli ya mazishi ya aliyekuwa Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania Kikosi namba 14 KJ PEMBA XPTE PETRO MASANJA NJANA ambaye alifariki dunia nchini Congo Aprili 6,2024 akiwa katika oparesheni ya Ulinzi wa Amani katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Mazishi ya askari huyo yamefanyila Aprili 14,2024
katika Kijiji cha Igegu Kata ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani
Simiyu.
0 Comments