Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mhe Musa Sima akikabidhi Shil 5000,000/= kwaajiri ya ujenzi wa shule katika ibada ya Swala ya Eid iliyofanyoka katika msikiti wa Qiblatain.
Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Singida Mjini Alhaj Hamisi Kisuke akiongea na waumini wa dini ya kiislam katika swal;a ya Eid.
Diwani wa kata ya Kindai Mhe Ommary Salum (kinyeto) akichangia ujenzi wa madarasa ya shule inayojengwa katika msikiti wa Qiblatain uliyopo Misuna mjini Singida.
Mwenyekiti wa Baraza kuu la Wislamu
BAKWATA wilaya ya Singida Hamisi Kisuke amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama
vya Wilaya kwa kudumisha ulinzi na usalama katika wakati wote wa mwezi mtukufu
wa Ramadhani kwani waumini wa dini ya kiislamu wameweza kuswali swala ya
Taraweeh inayoswaliwa wakati wa usiku bila changamoto.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa ibada ya
Eid El Fitri iliyofanyika katika viwanja vya msikiti wa QIBLATAIN uliyopo
katika kata ya Misuna Singida Mjini, ambapo Alhaj Kisuke amesema kuwa katika
mwezi huu hakukuwa na matukio ya kiuhalifu katika Manispaa ya Singida hasa
katika muda wa Swala hiyo.
Aliviomba vyombo hivyo kuendelea
kudumisha amani na utulivu wakati wote huku akitoa wito kwa waumini wa dini
hiyo kuendelea kutoa sadaka ili kuchangia ujenzi wa miradi ya maendelo ya
Msikiti huo ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule inayojengwa sasa.
Naye Imamu wa Msikiti wa Qiblatain
Idris Shaban aliwataka waumini wa dini ya kiislam waliyo jaaliwa kipato
kujitolea kuchangia kwani kutoa si utajiri ni moyo huku akiwataka wanawake
kuendeza tabia njema ya kujistili kimavazi na kimatendo hata baada ya mwezi huu
wa Ramadhani.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Singida
Mjini Mhe Musa Sima amewashukuru waumini wa dini hiyo kwa kuendelea kwa kushiriki
kuchangia ujenzi wa shule inayojengwa katika msikiti huo na kuunga mkono kwa
kuchangia shilingi laki tano (5,000,000)
Mhe. Sima aliishukuru serikali kwa kuendelea kusimamia vizuri
bei elekezi za bidhaa na kuwadhibiti wafanya biashara ambao hupandisha bei za
bidhaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Aidha Diwani wa kata jirani ya Kindai
Mhe Ommary Salum aliupongeza uongozi wa msikiti huo kwa kusimamia vyema ujenzi
wa shule hiyo huku akichangia Milango miwili, Mbao za kufunga lenta na Mchanga
lori tano
0 Comments