MAJERUHI WAONGEZEKA AJARI YA BASI SINGIDA.










 Basi la kampuni ya Rujiga Expres linalofanya safari za Mwanza na Dare es Salaam limepata ajali wakati likitokea jijini Dar es saalm kulekea Mwanza katika kijiji cha Malendi kata ya Mgongo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida na Kusababisha vifo vya watu 9 na wengine 10 kujeruhiwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe alipotembelea eneo la tukio na kuwatembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Iramba na hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, amesema majeruhi wanaendelea vizuri na matibabu kutoka kwa timu ya madaktari iliyotumwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.

Amesema timu hiyo ya madaktari bingwa inaendelea kusimamia matibabu ya majeruhi ambapo serikali inaendelea kuwasafirisha majeruhi ambao wamepata nafuu kurejea makwao.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Iramba Daniel Paul alithibitisha kupokea majeruhi wa ajali hiyo ambapo alisema walipokea majeruhi 12, huku majeruhi  9 walipatiwa huduma kituo cha afya Shelui na wengine  3 walipewa rufaa kupelekwa hospitali ya Wilaya Iramba ambapo wawili kati ya hao walifanyiwa upasuaji.

Amesema hospitali ya Wilaya ya Igunga ilipokea miili ya watu 7 ambapo miili 6 ni ya wanaume na mwanamke 1 na majeruhi 2 huku hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida ilipokea majeruhi 7 ambapo wawili kati yao walipoteza maisha wakiwa wanaendelea na matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Pipi Kayumba amesema ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya SANGOSTAN (T) LTD  lenye namba za usajili T315 CXX likitokea jijini Dar Es Salaam kuelekea jijini Mwanza kugonga lori aina ya DAF lenye namba T485 DDR na tela lake lenye namba T231 DSE mali ya kampuni ya GREENISH (T) LTD lililokuwa limeegeshwa  pembeni ya barabara likifanyiwa matengenezo.

ACP Kayumba amesema  Dereva wa basi hilo alitoroka baada ya ajali hiyo kutokea na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Hata hivyo mmoja wa majeruhi Athumani Rashidi aliyelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa aliishukuru serikali kwa kuimarisha huduma za afya na kuweka wataalamu ambapo wananachi wanapata huduma kwa wakati na kwa urahisi wanapopata changamoto.    

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments