Pamoja nakupoteza mchezo wa CRDB FEDERATION CUP bado benchi la ufundi Mnyama Simba limejipanga kuhakikisha lina
endeleza mpango wake wa kutwaa ubingwa
wa ligi kuu NBC PREMIER bara,Kuelekea
mchezo baina ya wenyeji Ihefu fc Dhidi ya Mnyama Simba Sport Club unaotarajiwa
kuchezwa Mjini Singida jumamosi ya April 13
CCM LITI STADIUM viongozi wa mabenchi ya ufundi wamekutana na
wanahabari katika ofisiu ya Bank ya NBC lililopo katikati ya Manispaa ya
Singida.
Wakijibu maswali ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika
kikao cha kikanuni ya ligi kuu NBC kocha msaidizi wa timu ya Simba Suleiman
Matola amesema kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa usajiri
wa timu ya Ihefu waliyoufanya katika dirisha dogo la usajiri la msimu huu.
Matola amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo
huo ili kuwapa moyo na morali wachezaji wao kwani wamejipanga kupata matokeo
mazuri kwani pointi tatu ni zamuhimu ,kwa
upande wake nahodha msaidi wa Simba
Mohamed Hussein amesema kuwa tunajua mashabiki wamesikitishwa na matokeo
yaliyopita lakini kwa mchezo huu tutahakikisha tunawafurahisha na kuwapa
faraja.
Naye kocha mkuu wa timu ya Ihefu fc Mecky Mexime amesema kuwa
Tunawaheshimu Simba kwani ni timu
kongwe na bora nchini lakini
tutahakikisha tunapata point tatu muhimu ikumbukwe kuwa kwa msimu huu
tumejiwekea mpango mkakati wa kuhakikisha tunajenga timu imara.
Aidha Mwakilishi wa wachezaji kutoka
timu ya Ihefu Morice Chuku amesema kuwa
wamejipanga kuhakikisha wanawafurahisha mashabiki wao kwani wapo katika
uwanja wa nyumbani na tunawaomba
wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao.
0 Comments