Picha kutoka maktaba yetu
Na Mwandishi wetu SingidaWAKALA wa barabara TANROADS mkoa wa
Singida,umetumia zaidi ya shilingi bilioni 69.7 kugharamia matengenezo ya
barabara kipindi kilichoishia karibuni,ili ziweze kupitika kwa urahisi.
Hayo yamesemwa na meneja TANROADS mkoani
Singida,injinia Msama Korasoni Msama,wakati akitembelea na kukagua uboreshaji
wa barabara za manispaa ya Singida.
Ameongeza kwamba katika kuhakikisha
barabara za mkoa zinapitika muda wote,wakala wa barabara-TANROADS,unaendelea na
operesheni ya kukagua maeneo korofi na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.
Injinia Msama amesema mafanikio makubwa ya
uboreshaji wa barabara za mkoa,yanachangiwa na serikali ya awamu ya sita chini
ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassani.
“Rais wetu mama Samia anatupatia fedha za
kutosha, kuhudumia barabara za mkoa wetu.Pia kusafisha/kuhudumia madaraja na
vivuko vyake.Kwa ujumla miradi tunayoihudumia mingi imekamilika”,alisema na
kuonge;
“Michache iliyobaki,inakaribia
kukamilika.Barabara ya Shelui-Sekenke ya kilometa 20,tutaijenga kwa kiwango cha
lami,ili ipitike kwa urahisi zaidi”.
Kuhusu barabara ya kuanzia Ilongero wilaya ya
Singida, hadi Hydomu wilaya ya Manyara itakayojengwa kwa kiwango cha
lami,wakati wo wote kuanzia sasa,zabuni yake itatatangazwa wakati wo wote.
Katika hatua nyingine,alisema mkandarasi mzawa
Janes Ezra anayemiliki kampuni ya Kangwa General supplies Ltd,ameifanyia
uboreshaji barabara inayopita ziwa Kindai na ziwa Monangi,inakaribia
kukamilika.Ambapo itapitika kwa urahisi”,amesema meneja huyo.
Akiongeza,Janes alisema kuwa wakandarasi
wazawa kwa ujumla wameonyesha wazi kazi wanaiweza,hivyo kilicho
mbele ni serikali na wadau mbalimbali,kuwaamini na kuwapa kazi za aina yo yote.
Aidha,Janes ametumia fursa hiyo kuonya kwamba
kuna uharibifu mkubwa wa barabara,unafanywa na watu wenye nia ovyo.Pia kuharibu
vyuma na alama za barabarani upingwe vita.
“Watu wa aina hii wakamatwe na
kufikishwa mbele ya mahakama.Huko wachukuliwe hatua
stahiki,zitakazowaongofya watu wengine, kufanya uharibifu”,amesisitiza.
Naye injinia Majengo wa kampuni ya Jam
engineer’s co,ltd,amewataka wakandarasi wenzake wazawa,wawe makini zaidi
kutekeleza kazi wanazopewa, ili waaminike na serikali
na wadau wengine.
“Rasi wetu mama Dk.Samia,anatupa fedha nyingi
na kwa wakati,sisi tulipe kwa kufanya kazi kwa kiwango kinachoaminika, na
wakati unaopangwa”,amesisitiza.
Ametoa wito kwamba miuondo mbinu ya
barabara itunzwe na kulindwa, na wananchi wasivamie maeneo ya
barabara.
Amesema kuwa TANROADS inatambua wazi kuwa
barabara ni muhimu kwa vile zinaunganisha watu.Hivyo ni farari kwetu kuzitunza.
0 Comments