SINGIDA.
Mkuu wa wilaya ya singida muhandisi
Paskasmuragili amewatahadhalisha wafanya biashara wenye tabia ya kukwepa ushuru
wa serikali kuwa waache mara moja, serikali ya wilaya ya Singida itaendelea
kuhakikisha inafanyaa ukaguzi wa kila gari la mizigo linalopita katika wilaya ya Singida na
litakaguliwa kama lina nyaraka halali za kusafirishia mizigo hasa mazao.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kukamata
maroli matano ya shehena ya mizigo ya
maharagwe,pumba na mchele yaliyokuwa yakitokea mkoa wa Kagera (bukoba) na kuelekea jiji la Arusha yakiwa hayana
nyaraka halali za malipo ya ushuru ya
serikali Zaidi ya shiringi 4,900.000/= huku kukiwa na udanganyifu wa baadhi ya
nyaraka.
Baada ya tukio hilo lililo tokea eneo
la njia panda kati ya wilaya ya Singida DC na manispaa majira ya saa 12.00
asubui mkatisha ushuru Bw Juma Athumani hakuridhishwa na nyaraka za mizigo hiyo
na kuamua kuyazuia magari hayo na kutoa taarifa kwa ungozi ambapo kamati ya
ulinzi na usarama ya wilaya ilifika na kujionea ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya
Singida na kuamuru malipo halali ya ushuru wa serikali yafanyike ndipo magari hayo yaendelee na
safari..
0 Comments