Mkuu wa Mkoa hapa Singida, Dkt. Bilinith Satano Mahenge,
ameanza ziara yake ya kukagua maeneo kadhaa yaliyochini ya halmashauri ya manispaa
ambapo leo ametembelea jala (Dampo) kubwa za taka ngumu, soko la vitunguu lililopo kata ya misuna na mradi wa kilimo cha umwagiliaji kisasida.
Dkt Mahenge amebaini changamoto zinazokabili
maeneo hayo na wananchi kwa ujumla ikiwa suala kubwa ni
hali ya usafi wa mazingira kutoridhisha kisha kumuagiza Kaimu Mkurugenzi wa manispaa,
Deus Luziga kuondosha taka ngumu zilizojaa katika Jala (Dampo) zote ndani ya
siku tatu pamoja na kuweka utaratibu wa usafi wa kila siku katika maeneo hayo
ili kuepusha hatari ya magojwa ya milipuko.
Akisisitiza katika hatua za kimaendeleo ili Singida
kufikia kuwa jiji, Dkt Mahenge amesema ni lazima miundombinu ya barabara na
sehemu zingeine kuimarishwa na akitolea mfano wa mtaa ya Sabasaba, barabara
zinahitaji kufanyiwa marekebisho ndani ya wakati.
Hata hivyo ameonesha kutoridhishwa na mwenendo
wa ukusanyaji wa mapato, katika halmashauri hapa singida na kusema kwamba‘matapo
mengi yanapotea kutokana na kukosa usimamizi bora hali inayopelekea upotevu
mapato ya serikali.’
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hapa
Singida Muhandisi Pascus Muragili akieleza
kuhusu tatizo la usafi wa mazingira ambalo liliibua sitofahamu kwa Afsa
mazingira Bi, Arafa Halifa, amesema manajimenti ya manispaa haina ushikiano
mzuri baina yao katika kutatua kero za wananchi.
Aidha kuhusu suala la soko
la vitunguu Msufini,Mkuu wa Mkoa, ametembelea na kujionea adha zinazolikabili eneo hilo ,na mwenyekiti wa
soko Iddi swalehe mwanja amesema licha ya kuwa na changamoto nyingi lakini
wameendelea kupiga hatua nzuri, na kuomba kutatuliwa kero zinazochelesha
maendeleo ya soko hilo.
Mkuu wa Mkoa Dkt. Bilinith Satano Mahenge ,anafanya
ziara ya siku mbili ,katika kutembelea maeneo tofauti tofauti yaliyopo ndani za
halmashauri ya manispaa ya Singida ili kujionea changamoto na shughuli
mbalimbali zinazofanyiwa na wananchi
katika maeneo hayo hususani katika vyanzo vya mapato.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Singida na mchumi wa Halmashauri Bw Deusi Luziga akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida katika kikao maalum.
kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida akimkaribisha katika jengo la ofisi za manispaa ya Singida ikiwa ni mara ya kwanza kufika katika ofisi hizo.
Ni baada ya kuingia ndani ya jengo la ofisi za manispaa ya singida na kubaini uchakavu wa jengo hilo .
baada ya kupata maelezo juu ya changamoto ya ukosefu wa gari la taka lililo alibika mkuu wa mkoa (Hayupo katika picha ) alifika katika gereji ya TEMESA kujionea hali ya gari hilo.
katikati ni mwenyekiti wa soko hilo akitoa maelezo mafupi juu ya hali ya biashara ya msimu wa vitunguu kwa mwaka huu.
pia mkuu wa mkoa alitembelea katika mradi wa kilimo cha umwagiliaji kilichopo katika kata ya Kisasida mjini hapa.
ni matenki makubwa ya kuhifadhiwa maji kwaajili ya kilimo hicho yaliyokaa kwa muda bila kutumika kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme.
0 Comments