Katika kuadhimisha siku ya mkulima
shambani shirika lisilo la kiserikali la
UN WOMEN kwa kushirikiana na FARM AFRIKA
na kwa insani ya KOICA waliandaa hafla fupi iliyofanyika katika shamba
darasa katika kijiji cha Mnang”ana kata ya Sepuka wilaya ya Ikungi mkoani
Singida.
Akiongea katika hafla hiyo mgeni
rasimi mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe Edward Mpogolo amefuraishwa na elimu
iliyotolewa kwa Zaidi ya wakulima miatatu hamsini katika vikundi mbalimbali
ikiwa ni ndani ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa mradi huo wa kilimo cha Alizeti
kupita mashamba darasa mbalimbali.
Bi Zainabu hamisi na Bw Ramadhani
hamisi Kitifui ni wanufaika wa mradi huo wanaelezea nanmna walivyoweza kuitumia
Elimu hio na kupata manufaa katika familia yao, "Tumenufaika sana na ujio wa shirika hili kwani wametupa elimu juu ya
kilimo bora cha Alizeti mimi na mkewangu tayali tuna shamba darasa hili hapa
unaona jinsi Alizeti ilivyostawi vizuri amesema mzee Ramadhani Kitiku".
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe,Edward Mpogolo akiongea na wananchi katika Hafla hiyo ya siku ya mkulima shambani.
0 Comments