MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI AENDELEZA JUHUDI YA KUWATUWA NDOO KINA MAMA JIMBONI.

Na Mwandishi wetu - Singida DC

Zaidi ya shilingi mili 88 zimetumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali  ya maji katika wilaya Singida Kaskazini hikiwa ni kwa Hisani ya Taasisi  ya Rehema Faundatin ya nchini Uturuki  taasisi kwa kushirikiana na  Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini Mhe Ramadhani Ighongo,miradi hiyo ya maji iliyojengwa katika kata nne za Kinyamwenda,Makhandi,Makuro na Itamka. 

Akiogea katika uzinduzi wa kituo kipya kilichopo katika kijiji cha Itamka kata ya Mrama BI Zainabu Ghamze amesema kuwa “UMUDA KONSANLAR "ni umoja wa mashirika yaliyopo nchini Uturuki yenye lengo la kutoa misaada kwa jamii mbalimbali tumefurahi sana kuwa hapa leo”.

Naye naibu waziri wa maji Muhandisi Meryprisca Mahundi akiongea baada ya uzinduzi wa kisima hicho cha Itamka katika mkutano wa hadhala uliyofanyika katika shule ya msingi Itamka pamoja na kuipongeza taasisi ya UMUDA KONSANLAR ya Uturuki pia amewataka wanchi kuitunza miundombinu hiyo ya maji kwani ni urithi wa vizazi vijavyo pia, “ niwaombe wakazi na wanchi wa vijiji vyote vinavyo jengewa miradi ya maji wilayani hapa na kwingineko kwa ujumla kuitunza miradi hiyo kwani ni urithi wetu wa vizazi vijavyo kwani miradi hiyo inatumia fetha nyingi sana. 

Awali akimkaribisha naibu waziri wa maji kuongea na wananchi wa kijiji hicho kuongea mbunge wa jimbo hilo la Singida kaskazini ameiomba serikali kupitia wizara yake kusaidia usambazaji wa maji hayo kutoka katika DP hiyo yenye uwezo wa kutoa maji kwa saa moja lita miasaba hamsini ili kuweza kusaidia wananchi wa  maeneo mengine ya karibu na kisima hicho chenye huwezo mkubwa wa kutoa maji.

kulia ni naibu waziri wa maji Muhandisi, Meryprisca mahundi na wa kawanza kushoto ni mbunge wa jimbo hilo  mhe, Ramadhani Ighondo wakimtua ndoo mama baada ya uzinduzi wa DP mpya ya maji katika kijiji cha Itamka.

kushoto mwenye kilemba ni Bi Zainabu Ghamze kutoka taasisi ya Rehema Faundation ya nchini uturuki akiwa na naibu waziri.
Naibu waziri wa maji akiongea na wanachi katika mkutano wa hadhala.

mhe, Mbunge na Diwana wa kata ya Mrama wakicheza ngoma ya kinyaturu.
Mhe,Ramadhani Ighondo mbunge wa jimbo hilo akingea na wananchi .

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments